BAADA YA MIAKA 31 MAREKANI KUKOSA FAINALI ZIJAZO ZA KOMBE LA DUNIA

Pulisic and Michael Bradley can't believe their luck after the surprise defeat on Tuesday
Licha ya kutofanya vyema katika fainali nyingi za kombe la Dunia lakini mara zote timu ya taifa ya Marekani imekua ikishiriki katika fainali za kombe la Dunia tangu ilipoingia mwaka 1986 lakini fainali zijazo zitakazofanyika Russia marekani itabidi watazame tu kwenye luninga baada ya timu yao ya taifa kushindwa kupata nafasi.

Marekani ilikutana na kichapo cha kushangaza cha bao 2-1 toka kwa Trinidad & Tobago nchi ya mwisho katika ukanda wa bara la Amerika ya Kaskazini.

Matokeo hayo yanaifanya Mexico kuongoza kundi hilo ikiwa na pointi 21 ikifatiwa na Costa Rica wenye pointi 16 na Panama ni ya tatu ikiwa na pointi 13 huku Honduras ikishika nafasi ya nne na kupata nafasi ya kucheza mechi ya mtoano.

Hakuna aliyetegemea kama Marekani ingeshindwa kufuzu kwani ilikua inahitaji pointi moja tu ikiwa na pointi zake 12 kwakua ilikua na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa lakini pointi hiyo moja ikawa ngumu kupatikana ugenini.

from WAPENDA SOKA
Soma Zaidi

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini