MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191

 

 

NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MAKAMBAKO
KUKAMILIKA
kwa Mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 220kV, na
usambazaji umeme vijijini kutoka Makambako-Songea kupitia Njombe, unatarajiwa kuondoa
kabisa tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa mijini na
vijiji vipatavyo 191, Meneja wa Mradi huo Mhandisi Didas Liyamuya,(pichani juu), amesema leo
Jumanne Oktoba 10, 2017 wakati wa ziara ya Wahariri wa vyombo vya habari
nchini.
Sambamba
na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pia utahusisha upanuzi wa kituo cha
kupoza umeme cha Makambako cha msongo wa umeme wa kilovolti 220/132/33Kv, na
ujenzi wa vituo vingine vipya viwili, vya Madaba na Songea vya msongo umeme wa kilovolti
220/33kV, halikadhalika ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa
kilovoti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa hiyo alisema
Mhandisi Liyamuya.
Akifafanua
zaidi, katika mkoa wa Njombe, umeme utasambazwa katika maeneo ya Makambako na
viunga vyake, Njombe yenyewe, na Ludewa, wakati mkoa wa Ruvuma umeme
utasambazwa katika mji wa Songea na vijiji vilivyo katika wilaya ya Mbinga,
Namtumbo na Madaba, na kuongeza kuwa umeme utakuwa wa msongo wa kilovolti 33 pamoja
na ujenzi wa mawasiliano “OPGW”.
“Lengo
la mradi huu ambao unafadhiliwa na Serikali ya Swedena kupitia Shirika lake la
Misaada ya Kimaendeleo SIDA, Serikali ya Tanzania na Shirika la Umeme Nchini,
TANESCO, ni kuboresha hali ya upatikanaji umeme katika maeneo ya uzalishaji na
majumbani.” Alifafanua.
Wahariri
hao walipata fursa ya kutembelea eneo la upanuzi wa kituo cha Makambako ambapo
walishuhudia kazi ya kujenga misingi ya mitambo ikiwemo Slope protection. Pia
walijionea kazi ya kufunga transfoma kwenye maeneo kadhaa ya Makambako ikiwemo
eneo la Lyamkena.
Mhandisi
Liyamuya alibainisha kuwa awamu ya kwanza ya mradi wa kusambaza umeme
utakamilika Desemba 2017 wakati awamu ya pili utakamilika Novemba 2018.
“Hadi
leo hii Oktoba 10, 2017, mradi umekamilika kwa asilimia 63 kwa upande wa mkoa
wa Ruvuma na asilimia 39.5 kwa upande wa mkoa wa Njombe na kazi kubwa
iliyofanyika ni ubainishaji wa maeneo ya kupitisha laini (njia ya umeme),
ubunifu wa jinsi muundo wa njia hiyo utakavyokuwa, ufyekaji wa njia za
kupitisha laini, ununuzi wa vifaa pamoja na kusimamisha nguzo za msongo wa 33kV
na 400V na kusambaza nyaya, na usimikaji wa Transofa.” Alisema.
Hata
hivyo Mhandisi Lyamuya alieleza masikitiko yake kwa baadhi ya watu kuchoma moto
ovyo misitu ambapo baadhi ya nguzo zilizosimikwa katika kipindi hiki cha mradi
zimeungua.
“Nitoe
rai kwa watanzania wenzangu, Serikali inafanya juhudi kubwa kuwafikishia huduma
hii muhimu ya umeme, na mfahamu kwamba fedha za walipa kodi wa Tanzania
Shilingi Bilioni 7 zilitolewa kama fidia, iweje leo tuanze kufanya uharibifu
huo.?” Alihoji, na kutaka vimgozi wa serikali kwenye maeneo yote ya mradi
kuwahamasisha wananchi kutunza miundombinu hiyo ambayo inaligharimu taifa fedha
nyingi.

 

 Mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Lyamkena, mji wa Makambako mkoani Njombe, ambaye ni mteja mpya wa TANESCO, Bw.Thomas Kiwale, (kulia), akihakikiwa wakati wa zoezi la kuwahakiki wateja walioomba kuunganishiwa umeme kwenye eneo hilo, na afisa wa TANESCO, Bi.Atuokoe Mhingi, Oktoba 10, 2017
 Wahariri na mafundi wa TANESCO, wakipita chini ya moja ya transofa zinazoednelea kufungwa kwenye mji wa Makambako Oktoba 10, 2017.
 Baadhi ya wahariri wakisikiliza maelzo yaliyokuwa yakitolewa na Mhandisi Liyamuya(hayupo pichani), kuhusu utekeelzaji wa mradi huo walipotembelea eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza na kusafirisha umeme wa 220kV cha Makambako.
 Baadhi ya wahariri
na mafundi wa TANESCO, wakisikiliza maelzo yaliyokuwa yakitolewa na Mhandisi Liyamuya(hayupo
pichani), kuhusu utekeelzaji wa mradi huo walipotembelea eneo la upanuzi
wa kituo cha kupoza na kusafirisha umeme wa 220kV cha Makambako.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bil Leila Muhaji, akifafanua baadhi ya mambo ambapo alisema, ili kujenga uhusiano mwema na wananchi walio jirani na eneo la Mradi, wateja watatozwa kiasi cha shilingi 27,000 tu kwa kazi hiyo katika kipindi hiki cha utekelezaji wa mradi, na hivyo kuwataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme kwa faida ya taifa na wao wenyewe.
 Bi.Atuokoe Mhingi,kutoka TANESCO, akiendelea na zoezi la kuwahakiki wateja walioomba kuunganishiwa umeme kwenye eneo la Lyamkena, Makambako Oktoka 10, 2017.
 Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
 Mhariri wa Mwananchi Online Digital, Peter Nyanje, (kushoto) na Mhariri wa gazeti ka Majira, Bw. Mwafisi wakifurahia jambo.
 Mhariri wa gazeti la Nipashe, Bw. Joseph Mwendapole, (kulia), akionyeshwa moja ya minara ya kupitisha umeme wa 220kV nje kidogo ya Makambako.

 

 Kazi ya ujenzi wa msingi wa kufunga mitambo kwenye eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza umeme wa 220kV Makambako ikiendelea.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi. Grace Kisyombe wakijadiliana jambo.
 Meneja Mradi wa ujezni wa njia ya kusafirisha umeme kutoka kampuni ya Isolux,Bw.Elmensour,(kulia), akielezea jinsi kazi hiyo inavyoendelea
Wahariri kutoka kushoto, Peter Nyanje, Joyce Shebe na Nevile Meena

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini