MSEMENI VIBAYA TU RONALDO ILA ANAENDA KUTWAA TUZO YA TANO YA BALLON D'OR

Related image
Msemeni tu Ronaldo ila wanaogombania Ballon d'or wametangazwa na huenda akapata upinzani wa kitoto toka kwa Lionel Messi na Neymar ambao huenda wakawa washuhudiaji wa kiti cha mbele (V.I.P) na Camera zikawafuata kuwaangalia jinsi hali itakavowalazimu kumpigia makofi na kutabasamu wakati akichukua tuzo ya tano ya uchezaji bora wa Dunia. 

Tuzo hii ni muhimu sana kwa Ronaldo kuifikia Rekodi iliyowekwa na Muargentina Lionel Messi ya kushinda tuzo hiyo kwa mara ya 5 wakati Ronaldo ana tuzo 3 tu na machoni pa wengi ilionekana asingeweza kuifikia hii rekodi lakini jasho jingi alilolitoa na magoli ya kila aina zitampa tuzo yake ya 5 na kuifikia rekodi hiyo ya Messi huku kazi itakayokuwepo mbele ni kuweka rekodi yake binafsi endapo atakua na kiwango kama alichonacho kwa miezi 12 ijayo.

 Ronaldo amefanya kazi kubwa ya kuibeba timu yake ya taifa ya ureno (Portugal) katika harakati za kukata tiketi ya kwenda Russia katika fainali za kombe la Dunia akifunga magoli 15 na endapo atafunga goli 2 tu kwenye mechi ya leo dhidi ya Switzeland basi huenda si tu akaikatia timu yake tiketi lakini pia  kwa kuweka rekodi ya kua mchezaji aliefunga goli nyingi kwenye mechi za kufuzu kwa michuano hiyo katika bara la Ulaya na kuandika historia mpya barani humo.

Kwa hali ilivyo sasa Roberto Lewandowski ndiye mchezaji mwenye rekodi ya kufunga magoli mpaka sasa akiwa ameshafunga goli 16 kwenye mechi za kufuzu baada ya kuifunga timu yake ya Poland goli 1 jana na kuipeleka katika fainali zijazo nchini Rusia lakini Ronaldo ana mechi 1 ya kucheza na huenda akaweka rekodi yake leo dhidi ya Uswisi akiwa ameshafunga magoli 15 mpaka sasa..

. kwa kila kejeli, tusi ama jiwe analopigwa Ronaldo amekua mnyenyekevu na anawaumiza kwa vitu vyake machachari uwanjani, Mchezaji huyo bora wa dunia kwa sasa ana nafasi kubwa ya kua mchezaji bora wa dunia kwa miezi 12 ijayo na ameanza kupokea pongezi za awali za ushindi wake mkubwa ni vile matunda ya kiwango chake yamestawi sana basi kuna watu wanaendelea kumpiga mawe lakini kupingwa ni athali ndogo ndogo hasa ukiwa mchezaji bora wa Dunia.

Na Hofmann Maina (Member Wapenda Soka) 

from WAPENDA SOKA
Soma Zaidi

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini