SEKTA YA MBOGA MBOGA NA MATUNDA YAKIPAISHA KILIMO

DSC_0382

Na Mahmoud Ahmad Arusha

Serikali imesema kuwa sekta ya matunda na mbogamboga inakuwa kwa kasi na kuipatia fedha nyingi za kigeni tokea kuanzishwa kwake 2004 na kukisaidia kilimo kukuwa kutoka asilimia 6.4 hadi asilimia 11 na kuweza kukusanya dola za kimarekani 660 milion.

Hayo yamebainishwa kwenye hotuba ya waziri wa Kilimo Dkta Charles Tizeba   iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala kwenye mkutano wa wadau wa sekta hiyo unaofanyika kwa siku mbili jijini hapa.

Makala alisema kuwa Sekta hiyo imekuwa ikiajiri watanzania vijana million 2.4 na kuisaidia serikali katika mapambano ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na serikali imejikita kuisaidia sekta hiyo ili iweze kuondoa tatizo hilo la ajira kwa vijana kupitia kilimo ni sekta kubwa inayoweza kuwapa watanzania mafanikio.

“Mipango yetu kama wizara ni kuweza kuisaida sekta ya matunda mbogamboga na mauwa kuwa mkombozi wa kuinua kilimo hapa nchini na kuondoa Tatizo la ajira kwani sekta hii imeonyesha kuweza kuondoa tatizo hilo na kuwa mkombozi wa kuongeza pato la taifa” alisema Makala.

Nae Mkurugezi wa taasisi ya matunda na mbogamboga TAHA Jaqulien Mkindi alisema taasisi hiyo imejikita katika kutoa huduma za kiufundi na masoko kwa wakulima na imekuwa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwepo na usafiri wa uhakika wa kusafirisha mazao hayo kwenye nje kwani wamekuwa wakisafirisha mazao hayo kupitia uwanja wa ndege wa Jomo kenyata uliopo nchini Kenya.

Alisema kuwa sababu kubwa ni gharama kubwa za mafuta katika viwanja vyetu hapa nchini na kuiomba serikali kuisaidia sekta hiyo ilikuweza kuyafikia masoko kwa wakati pia akaomba serikali iweze kuisaidia vijana wengi kupata uwelewa wa kilimo hicho cha matunda na mboga mboga kuweza kuisaidia kukuza pato la taifa na kilimo kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege Hamza Johari alisema nafasi ya kushiriki mkutano huo wa wadau wa matunda na mbogamboga utasaidia kujua changamoto wanazokabiliana wakulima wa sekta hiyo ilikuondoa na kuweza kukabiliana na washindani wao kuweza kuliteka soko la usafiri wa anga.

Alisema kuwa washundani wao ndio watatoa mwanga wa wao kuweza kufanya vizuri ili wadau hao waweze kusafirisha mazao yao kupitia viwanja vya hapa nchini na kuacha kupeleka mazao yao kwa washindani wao nchi jirani ya Kenya.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini