SHINDANO LA STARTIMES KUSAKA VIPAJI VYA SAUTI LAFUNIKA JIJINI MWANZA

1

Shindano linalodhaminiwa na kampuni ya Star Media (T) Ltd wamiliki wa Chapa ya StarTimes, wikiendi iliyopita siku ya Jumamosi tarehe 7, hatua ya Usaili iliendelea jijini Mwanza, ambapo mchuano ulikuwa mkali haswa.

Jijini Mwanza usaili ulifanyika pale Rock City Mall, ambapo mamia, wake kwa waume na walemavu pia walifika kuonesha umahiri wao katika kuingiza Sauti. Usaili ulianza majira ya Saa tatu Asubuhi huku majaji wakiwa na wakati mgumu kuchagua wachache ambao wataingia hatua ya fainali baadaye mwisho wa Mwezi huu jijini Dar es Salaam.unnamed

Kutokana na ushindani mkubwa baina ya washiriki, majaji walipendekeza majina kumi na moja badala ya mnajina kumi kuingia raundi ya mwisho jijini Mwanza, washiriki wawili walipata Alama sawa hivyo wote wakaingia hatua iliyofuata. Licha ya ushindani huo mwisho wa Siku ni majina matano tu ndiyo yalibahatika kuingia hatua ya fainali.

Miongoni mwa washiriki hao ni msanii wa Muziki wa kizazi kipya “Pipi”. Pipi alionyesha uwezo mkubwa wa kuingiza sauti na hivyo kupata nafasi ya kuingia fainali ya Shindano hilo jijini Dar es Salaam mwisho wa mwezi huu.

Wikiendi hii ni zamu ya Dar es Salaam, usaili utafanyika katika fukwe za bahari, Coco Beach Siu ya jumamosi tarehe 14 mwezi wa 10. “Washiriki ambao wamekwishajiandikisha hadi sasa ni zaidi ya 700 na tunategemea wengine zaidi kwa muda uliobaki,” alisema Bi. Li Kun, ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko, Star Media (T) Ltd.

Huu ni msimu wa pili wa Shindano hilo la Kusaka vipaji vya Sauti katika tamthiliya na filamu za kigeni, Msimu wa kwanza ulifanyika mwaka jana ambapo idadi ya washindi kumi walipatikana na tayari saba kati yao wapo nchini China wakifanya kazi. Msanii wa maigizo, Nyamayao ni miongoni mwa washindi wa mwaka jana na tayari ameshatua nchini kwa ajili ya kutioa hamasa kwa watanzania kushiriki katika shindano hilo.

“Ni nafasi ya kipekee ya kutumia kipaji chako, kufanya kazi na kukitangaza Kisawahili kimataifa. Kwa muda mabao tumekuwa China, tumepata  nafasi ya kushiriki midahalo na makongamano mbalimbali ambayo yametuwezesha kuwasilisha Utamaduni wa kitanzania kwa Ulimwengu” alisema Nyamayao.

Star Media (T) Ltd kupitia nembo ya StarTimes ndio wamiliki na wadhamini wa shindano hili la vipaji vya Kuingiza Sauti.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini