SIMBA,STAND,SINGIDA ZAPIGWA FAINI MWAMUZI AENGULIWA KUCHEZESHA LIGI KUU

Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji (Kamati ya saa 72) imetoa adhabu kwa vitendo visivyokubalika kwa mujibu wa kanuni za ligi huku klabu ya Simba, Stand United na Singida United na mwamuzi mwana mama   Grace Wamara wakikumbwa na rungu hilo.

Simba imepigwa faini ya sh 500,000 (laki tano) kutokana na kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Septemba 21 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(14) ya ligi kuu, na adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14(49) ya ligi luu. Pia Kamishna wa mechi hiyo, Maliki Tibabimale amepewa Onyo kali kwa kutoripoti kitendo hicho cha Simba.

Kwa upande wake Wamara ameenguliwa kuchezesha ligi kuu ya  kwa kukosa umakini na kutomsaidia Mwamuzi, hivyo kusababisha akubali bao lenye utata la Stand United dhidi ya Mbeya City.

Wamara alikuwa Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili kwenye mechi hiyo namba 31 iliyofanyika Septemba 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na wenyeji Stand United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Klabu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na wachezaji wake kuvaa jezi zenye namba tofauti na zile zilizosajiliwa. Wachezaji hao walivaa namba tofauti kwenye mechi namba 40 dhidi ya Simba iliyofanyika Oktoba 1 mwaka huu Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Singida United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani kushangilia ushindi baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyofanyika Septemba 23 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Nayo Stand United imepigwa faini ya jumla ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi dhidi ya Mbeya City na Simba, zote zilichezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Adhabu hiyo ambayo ni sh. 500,000 (laki tano) kwa kila mechi imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.


from WAPENDA SOKA
Soma Zaidi

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini