UFUNGUZI WA MKUTANO WA 6 WA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI UNAOFANYIKA MJINI ARUSHA

No. 1

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Horice Kolimba akifungua Mkutano wa 6 wa Mwaka wa Utawala Bora  Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Maudhui ya Mkutano huo ni Kuimarisha Demokrasia kwa ajili ya kuwezesha  Mtangamano  Endelevu.

Mada katika mkutano huo ni pamoja na : Kuheshimu Haki za Binaadamu na Nguvu ya Umma; Chagamoto na utekelezaji wake. Burundi inawasilisha mada hiyo.

Aidha Kenya itawasilisha mada ya Kuimarisha Uwajibikaji katika Utawala wa Sheria.

Rwanda itawasilisha mada ya Uadilifu wa Maadili katika Kampeni za Kisiasa na Tanzania itawasilisha mada ya Kuimarisha Mtangamano kupitia Uwazi katika Usimamizi wa Mikataba ya Ununuzi wa Umma.

Mkutano huo wa siku mbili umeanza leo Jumanne na utamalizika kesho Jumatano.

No. 2

Mbele katika picha Mhe. Said Hassan Said, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye ni Mkuu wa Ujumbe wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Mkutano huo.

No. 3

Baadhi ya Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mutano wa 6 wa Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Mkutano huo leo jijini Arusha.

             Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikian wa Afrika Mashariki

                                             Othman M. Othman

 


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini