VIKWAZO VYA KIBIASHARA KATI YA ZANZIBAR NA TANZANIA BARA VYAENDELEA KUFANYIWA KAZI

index

Na Ali Issa  Maelezo

Waziri wa Biashara,viwanda na masoko Balozi Amina Salum Ali amesema vikwazo vya kibiashra baina ya Zanzibar na Tazania bara inaendelea kufanya mazungumzo na watendaji wa taasisi za Tanzania bara ili kuondosha vikwazo vya kibiashara baina ya pande hizo mbili.

Hayo ameyasema leo huko baraza la wakilishi chukwani katika kikao kinacho endelea barazani hapo wakati akijibu suali la mwakilishi wa jimbo la paje Jaku Hashim Ayuob alietaka kujuwa kwanini hivi karibuni serikali ya jamuhuri ya mungano wa Tanazinaia ilifanya mazungumzo na Serikali ya Kenya kutatua changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo na mazungumzo yao yamekuwa ya mafanikio  makubwa kwa kupitisha didhaa baina ya Kenya na Tanzania zimetatuliwa .

Je,kwanini kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara kwa mda mrefu kumekuwa na changamoto za wafanya biashara wa Zanzibar kufanya biashara bila ya Bughudha Tanzania bara licha ya jambo hilo kuwa la muda mrefu bado changamoto hizo zipo kwa miaka mingi zikiwa nchi zao zina udugu wa damu kwa mda mrefu.

Waziri alisema vikwazo vya kibiashara baina ya Kenya na Tanazania ,Kenya iliwekea vikwazo Tanazania katika bidhaa ya unga na bidhaa ya gesi na hivyo kusababisha usumbufu wa biashara kwa upande wa Tanzania.

Alisema na kwa upande wa Tanzania nayo iliwaekea vikwazo Kenya katika bidhaa za maziwa na sigara kuingia ndani ya soko la Tanzania nayo ikawaekea vikwazo yasiingie Tanzania ,baada ya jambo hilo kupelekwa ngazi za juu viongozi wakuu wanchi hizo mbili wamekubaliana kuondolewa vikwazo baina ya nchi zao mbili ,na makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano uliofanyika septemba 8, 2017 mwaka huu.

Alisema kwa upande wa vikwazo vya kibiashara baina Tanzania Bara na Zanzibar  wizara yake inaendelea kufanya mazungumzo  na watendaji wa taasisi za bara ili kuondosha vikwazo baina ya nchi hizo mbili.

 Waziri huyo amesema hivi karibuni wizara yake ilikuwa na kikao na wizara ya viwanda ili kuangalia matatizo yanayo wakabili wafanya biashara wanchi zao mbili.

Aidha waziri huyo alisema kuwa kupitia kamati ya kusimamia masuala ya vikwazo vya kibiashara visivyo kuwa vya kiushuru kamati hiyo imeundwa ili kufuatilia changamoto hizo ili hatimaye kuendelea kuzitatuwa na kuzipatia ufumbuzi muafaka.

Hata hivyo waziri huyo alisema suala la vikwazo vya kibiashara baina yao litazungumzwa kwenye vikao vya mashirikiano baina SMT na SMZ vinavyo fuata.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini