HUYU NDIE KOCHA MPYA SIMBA

Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.

Taarifa inasema kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na huku akisaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu.

Inadaiwa Lichantre amewahi kufundisha vilabu kadhaa duniani ikiwemo Timu ya Taifa ya Cameroun iliyotwaa ubingwa wa Africa mwaka 2000.

Pia aliwahi kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na kua kocha bora barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi

Leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikiumana na Singida United kwenye Uwanja wa taifa.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini