MBUNGE MSIGWA ALISHUKIA JESHI LA POLISI,SOMA HAPO KUJUA

Iringa. Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mhe. Peter Msingwa amelijia juu Jeshi la Polisi Iringa Mjini kufuatia zoezi la kamata kamata linaloendelea katika oparesheni ya kuwasaka wale wote waliohusika na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba ya kiongozi mmoja wa UVCCM wilayani hapo.
Akiandika kwenye Ukurasa wake wa tweeter mapema leo Alhamisi Januari 18, 2018, Msigwa amewataka Polisi kuacha mara moja kuwakamata vijana wa Chadema wanaodhaniwa kuhusika na tukio hilo akidai chama hicho hakina desturi ya kulipiza visasi vya damu.
“Polisi Iringa acheni mara moja kamata kamata ya Vijana Iringa Mjini kwa tuhuma za kuchomwa nyumba Moto na kubomolewa nyumba. Chadema haina visasi vya damu ktk struggle ya Demokrasia Nchini. Kuhusisha uharibifu wa aina hii na siasa ni kukosa weledi na maarifa ktk uchunguzi” ameandika Msigwa.
Katika hatua nyingine Msigwa amewasihi Polisi kuacha kujikita kwenye kile alichokiita investigation analysis na badala yake wajikite kwenye intelligence analysis ambayo hutumika kubaini wahusika halisi wa matukio mbalimbali ya uhalifu.
“Pamoja na kwamba zote ni kazi za polisi,lakini kuna tofouti kubwa sana kati ya intelligence analysis na investigation analysis! Kwa Bahati mbaya polisi wetu wanajikita zaidi kwenye investigation analysis! Hii mara nyingi huumiza watu wasiohusika, na kuwaacha wahusika!”amesema Msigwa.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini