Ndugulile azindua SACOSS ya Wanawake Jijini Mbeya

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile  amezidua Saccoss ya Wanawake katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ajili ya wajasiriamali wadogowadogo ili kuweza kutatua changamoto zao na kuwawezesha kupa mbinu mbalimbali za kufanikisha matarajio yao na kupata maendeleo.

Ameizindua Saccoss  hiyo Mkoani Mbeya  wakati akiitambulisha  Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika Manispaa ya ya Jiji la Mbeya yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana  kati yao wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo linaenda sambamba na uwezeshwaji wa wanawake  katika  kuwashirikisha wanawake wenyewe katika kuibua miradi na kuanzisha shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya fursa na weledi wa wananchi wenyewe.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake kuwaweza kuanzisha vikundi vitakavyoanzisha viwanda vidogo vidogo na kuzalisha bidhaa zitakazo uzwa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya na hivyo kuutangaza mkoa kupitia bidhaa zilizozalishwa kwa kutumia ubunifu na rasilimali zilizopo.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saxccoss ya Wanawake ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali kiuchumi na kuwashirikisha wajasiliamali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia ujuzi, mbinu, maarifa, taarifa za soko na upatikanaji wa mikopo na vifaa.

“Niseme uzinduzi wa Saccoss hii kwa ajili ya wajasiriamali ni muhimu kwenu wanawake wajasiriamali na hata wale ambao wanaanza na kwa asilimia kubwa itasaidia kuibua wanawake ambao hawakuwa na mitaji ya  kufanya shughuli zao pamoja na kuwawezesha kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati” alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi  amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara na kusaidia kuhamasisha Halmashauri kutenga asilimia 10 kwa wanawake na vijana ambazo zitatumika kama mtaji wenye masharti nafuu wa kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mweyekiti wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya  Bw. amesema kuwa programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saccoss ya wanawake itasaidia kuwainua wanawake ikiwa halmashauri zitashirikiana na wadau wa maendeleo kuwawezesha wanawake kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji na kumwahakikishia Naibu Waziri kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kufanikisha masuala ya maendeleo katika Mkoa wa Mbeya.

Mmoja wa Wanawake wajasiliamali Manispaa ya Jiji la Mbeya Bi. ameishukuru Serikali kwa kuzindua Progarmu ya kikundi Mlezi na kuanzishwa kwa Saccoss hiyo utakaowawezesha wanawake kusaidiana  katika kuanzisha na kuboresha biashara ambazozitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

The post Ndugulile azindua SACOSS ya Wanawake Jijini Mbeya appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini