OKWI AREJEA NA BAO 2 SIMBA IKIPIGA SINGIDA UNITED 4G

Vinara wa ligi kuu Soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kubwa katika ngazi ya klabu nchini Tanzania Kwa kuifunga Singida United bao 4-0.

Mshambuliaji kipenzi cha mashabiki wa Simba Emmanuel Okwi aliifungia Simba mabao mawili akirejea dimbani Kwa Mara ya kwanza baada ya kuwa nje ya uwanja Kwa muda mrefu na alianzia benchi katika mechi ya Leo na akaingia kuchukua nafasi ya Mdhamiru Yasin aliyeumia.

Shiza Kichuya alitangulia kuifungia Simba bao la mapema kabisa baada ya beki ya Singida United kushindwa kuokoa mpira wa adhabu ndogo wa Mwinyi Kazimoto.

Mabeki wa Singida United walionekana kushindwa kabisa kuikabili Simba ambayo ilikua ikitumia mfumo mpya wa kuchezesha  mabeki watatu, Viungo watano na washambuliaji wawili na kuruhusu kufungwa bao la Pili likifungwa na beki wa Simba Asante Kwasi baada ya kutumia pasi ya Hamis Ndemla.

Simba sasa imefikisha pointi 29 ikiongoza ligi hiyo na hii inafatia Azam FC kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Maji Maji ya Songea katika mchezo uliopigwa mchana wa Leo.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini