SERIKALI YAJA NA MUONGOZO WA KUPAMBANA NA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeandaa Muongozo wa matibabu nchini na orodha ya dawa zote muhimu ili kuepukana na tatizo la usugu wa vimelea vya dawa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote muhimu uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Ni muhimu kila kituo cha afya kuwa na dawa za kutosha, vifaa na vifaa tiba lakini ni lazima tuzingatie muongozo wa matibabu na orodha ya dawa kulingana na ugonjwa fulani ili kuepuka tatizo hili” alisema Waziri  Ummy

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Muongozo huo umezingatia vigezo vyote vya kuweka dawa ambazo zilikuwa hazipo katika ngazi ya  zahanati na  vituo vya afya ambazo zimepata uthibitisho kutoka Shirika la Afya la Dunia (WHO).

Aidha Waziri Ummy amewapiga marufuku Bohari Kuu ya dawa ya Taifa MSD na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) kuagiza na kuandika dawa zilizo nje ya muongozo uliozinduliwa leo ili kuondoa matumizi ya dawa yasiyo sahihi.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kila kituo cha afya ni lazima kiongozwe na Tabibu na sio vinginevyo ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika kituo cha afya husika.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya amesema kuwa itafika kipindi vituo vya afya ambavyo havikizi vigezo vitafungiwa ili kuepuka usababishwaji wa vifo visivyo vya lazima kwa watanzania.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi amesema kuwa muongozo wa kutibu magonjwa mbambali  umezingatia Orodha ya dawa ambazo zitakuwa zinatumika nchini kwetu kama dawa muhimu za kutibu magonjwa hayo.

The post SERIKALI YAJA NA MUONGOZO WA KUPAMBANA NA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA. appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini