Dar es Salaam. Mazungumzo kati ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza na mwanamuziki Giggy Money kuhusu picha za nusu utupu na kufungiwa kujishughulisha na sanaa yamekwama baada ya wote wawili kuugua.
Waziri Shonza akizungumza na Mwananchi jana Jumanne jioni amesema ameshindwa kukutana na msanii huyo kama walivyopanga kutokana na matatizo ya kiafya lakini amesisitiza kuwa agizo lake lipo pale pale.
Amesema alimwagiza msanii huyo afike ofisini kwake na kwamba atakutana naye pale hali yake kiafya itakapokaa sawa.
Kwa upande wake Giggy Money ambaye jina lake halisi ni Gift Stanford amesema ameshindwa kufika ofisini kwa waziri huyo kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.
Giggy Money ambaye awali alifika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) badala ya ofisini kwa waziri huyo kama lilivyokuwa agizo, alisema alipanga kuonana naye wiki iliyopita lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hakuyaweka bayana.
Sponsored by
ZAMOTO MEDIA
0 Comments