UZITO SALAMA WA MWILI NI UPI?

bmi-4
Kumekuwa na muamko mkubwa kwa watu kupenda kujua na kupima uzito wao. Jambo hilo ni zuri sana, hususan kwa kuzingatia kwamba uzito wa mwili una mchango mkubwa katika afya na magonjwa na hata hali ya mwili kwa ujumla. 

Watu wengi hupima uzito na kujua kilo zao tu. Kilo 50, kilo 65, kilo 80, kilo 100 na kadhalika. Je, hiyo inatosha? Jibu ni HAPANA!
bmi-4 Zaidi ya kujua uzito wako ni kilo ngapi inabidi ujue uzito wako unamaanisha nini. Je, ni salama au sio salama? Unahitaji kuongezwa au kupunguzwa? Hilo tunalijua kwa kupitia kujua uwiano wa uzito  wa mwili (Kilo) kwa Urefu wa mwili (Mita), yaani BMI (Body Mass Index). Soma kwa makini kuhusu BMI, maana hapa ndo maana halisi ya uzito wako ipo.
BMI NI NINI?                                                   bmi-2
BMI ni kifupi cha maneno “Body Mass Index”. Ni kipimo cha uwiano wa uzito wa mwili na kimo cha mwili. BMI ndiyo hujulisha kama uzito wako ni wa kawaida, salama au sio salama. Pia inaonesha ni salama au sio salama kwa kiasi gani.
Ili kupata “BMI” yako fanya kama ifuatavyo:
i. Pima uzito wako (Uwe katika Kilo). Kwa mfano, kilo 60
ii. Pima kimo chako (Kiwe katika Mita). Kwa mfano, Mita 1.5. Kisha zidisha kimo chako kwa kimo chako tena, kwa mfano kwa kimo cha Mita 1.5 basi itakuwa ni Mita 1.5 x Mita 1.5 = Mita za mraba 2.25.
iii. Gawanya uzito wako kwa Mita za mraba za Kimo chako. Kwa mfano wa kilo za hapo juu na urefu wa hapo juu itakuwa  = Kilo 60 / Mita za mraba 2.25
60 / 2.25 = 26.67
Hapa maana yake ni kwamba BMI ya mtu huyu ni 26.67
Sasa pima uzito wako na urefu wako (Kimo). Kisha tafuta BMI yako.
Umepata ngapi?
bmi
MAANA ZA BMI
BMI ni namba zinazoonesha uwiano wa uzito wa mwili na kimo cha mtu. Ili kuwa na afya njema na kutokuwa katika hatari ya kupata matatizo na magonjwa kama vile Kisukari, Shinikizo la damu, Uzito uliopitiliza, Matatizo ya viungo na miguu, Matatizo ya Moyo na mengineyo mengi basi ni vyema mtu awe na BMI ya kawaida. Tafsiri za BMI ni kama ifuatavyo:
bmi-3

  • Chini ya 18.5 = Uzito mdogo
  • Kuanzia 18.5 mpaka 24.99 = Uzito wa kawaida na salama kwa afya
  • Kuanzia 25 mpaka 29.99 = Uzito mkubwa
  • Kuanzia 30 na kuendelea = Uzito mkubwa sana. Sio salama kwa afya
Kimsingi, BMI yako inabidi iwe kati ya 18.5 mpaka 24.99. Vinginevyo uzito wako sio mzuri, jitahidi kuupunguza au kuuongeza mpaka ufikie hapo.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini