Wana CHADEMA Wenzangu, Mara hii Tumesahau ya November 26 na ya Chaguzi za nyuma?

Maswali yangu ni haya:
1.Tume ya Uchaguzi imebadilika?
Kama haijabadilika,tumejipangaje?

2. Wakurugenzi na watendaji wa Kata watakuwa fair safari hii?
Kama hawatakuwa fair,tumejipangaje?

3. Tumejipanga vipi kukabiliana na wale wavaa sare tunaowalalamikia kila kukicha?


4. Tumejipanga vipi kukubaliana na maagizo kutoka juu?


5. Je, mnajua jamaa zetu safari hii watakuja na mbinu gani?

6. Chama chetu kimejipangaje japo inaweza kuwa ni siri yao?

7. Tunaikabili vipi sheria ya mita 200?

8. Tumejipanga na tuko tayari kukusanya na kuchukua ushahidi kwa gharama yoyote ile na katika mazingira yoyote yale?

9. Tuna uhakika Mawakala wetu wote hakuna watakoweza kurubuniwa na vipande 30 vya fedha?

Mwisho:
Kwa kuwa tumekubali kuingia katika kinyang'anyiro hiki,nashauri wabunge wa chama wa mikoa ya Dar-es-Salaam na Kilimanjaro pamoja na wa mikoa ya jirani(kama ikibidi) na hata vingozi wa juu wa chama kama itabidi pia, ndio wawe mawakala kwenye huu uchaguzi.

Wagombea/Mgombea mzuri ni jambo moja na kushinda uchaguzi ni jambo lingine kwa nchi zetu hizi za kiafrika.

Salary Slip


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini