Audio: Beatrice Mwaipaja – Dhahabu

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Beatrice Mwaipaja ameachia wimbo wake mpya uitwao Dhahabu, ukiwa umefanyika chini ya mikono ya prodyuza Maka-Rhythm.

Dhahabu ni wimbo uliobeba ujumbe wa kukupa hamasa na nguvu ya kuendelea mbele hata kwa kipindi ambacho unahisi kuchoka na kukata tamaa ndani ya nafsi yako, kupitia wimbo huu mwimbaji Beatrice Mwaipaja anatukumbusha kuwa kila pito tunalopitia ni ishara ya ushindi kwa siku zijazo hivyo hutupaswi kukata tamaa kwakuwa Mungu alituumba kwa mfano wake hivyo sisi ni mfano wa thamani ya dhahabu ambayo haiwezi kung’aa mpaka ipitishwe kwenye moto mkali, vivyo hivyo katika maisha yetu ya kawaida tunakuwa tunapitia mapito magumu sana ambayo yanaweza kusababisha kutokuona ukuu na upendo wa Mungu kwetu lakini tunapaswa kutambua kuwa ushindi wetu ni lazima kwa yeyote amtegemeaye Mungu, kwakuwa wewe ni Dhahabu.

Kwa mujibu wa Beatrice Mwaipaja alisema haya kuhusu ujumbe ulio katika wimbo huu:

Huu ni wimbo wangu mpya ambao unaitwa DHAHABU, ni wimbo wenye kutia Moyo kwa ambao wamedharaulika na kuteswa na maneno ya Binadamu. Kama Dhahabu uwa inapita kwenye Moto ili kuwa Dhahabu hivyo nasi lazima tupite kwenye magumu ili tuifikie Ile NEEMA ambayo Mungu ametuandalia.” – Alisema Beatrice Mwaipaja

Nina hakika utabarikiwa na kuinuliwa, Karibu kusikiliza na kupakua pia usiache kujiunga na channel yake ya YouTube.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko mbalimbali na kama unahitaji kufanya kazi na mwimbaji Beatrice Mwaipaja wasiliana naye kupitia:
Namba za simu/WhatsApp: +255 654 345 737
Facebook: Beatrice Mwaipaja
Instagram: @beatrice_mwaipaja
YouTube: Beatrice Mwaipaja

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

share

The post Audio: Beatrice Mwaipaja – Dhahabu appeared first on Gospo Media.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini