Msanii wa muziki Tanzania, Diamond Platnumz ameamua kuweka wazi sababu ya migogoro yake na baadhi ya vyombo vya habari nchini ambapo amesema kuwa ni sababu za kimaslahi tu na sio kitu kingine.
Akizungumza kwenye kipindi cha Playlist kinachorushwa na Times FM, Diamond amesema kuna kituo ambacho huwa kinaandaa matamasha yake mikoani na kilitaka kumtumia Harmonize kwenye show yao bure lakini alipowataka japo walipie pesa kidogo ndipo migogoro ya kimaslahi ikaanzia hapo.
Diamond amesema kuna kituo cha Radio na TV hapa nchini kina miaka minne mpaka sasa hakijawahi kupiga nyimbo zake baada ya kukataa kushiriki kwenye tuzo ambazo ziliandaliwa na kituo hicho.
Sponsored by
ZAMOTO MEDIA
0 Comments