DKT. Mwakyembe Afungua Mkutano wa 14 wa Maafisa Mawasiliano wa Serikali Jijini Arusha

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaagiza Maafisa Habari wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za serikali huku akiwataka kuzingatia malengo ya kitaifa waliyojiwekea katika kikao kilichopita.

Mbali na agizo hilo Dkt. Mwakyembe pia amesema serikali haitawavumilia maafisa habari ambao hawatambui wajibu wao  huku akiwafananisha na maafisa habari hewa  ambao wanageuza tovuti za Serikali kuwa magofu badala ya kuwa na habari mbalimbali zenye tija na maendeleo kwa taifa la Tanzania.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo  wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikali, kinachofanyika katika Ukumbi wa mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha kinachowakutanisha zaidi ya Maafisa Habari zaidi ya 300 kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika kikao hicho kinachoenda sambamba na Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO)kinafanyika wakati kukiwa bado kuna changamoto katika kada ya maafisa Habari wa taasisi za Umma ikiwemo uharaka wa ufikishaji wa taarifa za serikali kwa umma .

Katika mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amewakumbusha washiriki wa mkutano huo kuenenda kimkakati huku akitoa nukuu za mcheza filamu Mashuhuri nchini Marekani ,Anord Schwazniger .

Naye Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa  Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez amesema serikali ina umuhimu mkubwa wa kufundisha na kuhabarisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zinazo iunganisha Dunia .

“Umoja wa Mataifa unaiona Tanzania ya leo na kesho yenye mafanikio mengi sana, Demkorasia, kufikia uchumi wa kati, Elimu Bure, kupiga vita rushwa ni kati ya vitu vinavyoipa Tanzania sifa ya nchi iliyo tayari kuleta maendeleo ya nchi kwa ajili ya wananchi.” alisema Rodriguez.

Katika mkutano huo TAGCO ambacho ni chama kisicho cha kiserikali (NGO) kikiwa na madhumuni ya kukuza Mawasiliano na kuongeza Usambazaji wa  Taarifa ndani ya serikali na kati ya serikali na Wananchi  kimekabidh vyeti kwa Wadhamini wa mkutano huo ikiwemo Kampuni ya Clouds Media Group.

The post DKT. Mwakyembe Afungua Mkutano wa 14 wa Maafisa Mawasiliano wa Serikali Jijini Arusha appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini