HARRY KANE, SALAH NA AGUERO KUVUNJA REKODI YA RONALDO MSIMU HUU?

Imepita miaka 10 tangu CRISTIANO RONALDO kufunga mabao 42 akiichezea Manchester United msimu wa mwaka 2007/2008 kwenye mashindano yote.

Msimu ambao Ronaldo alikua pia mfungaji bora wa ligi kuu ya England akiwa na magoli 31, Goli 8 katika ligi ya Mabingwa Ulaya na goli 3 katika kombe la FA.

Tangu wakati huo mpaka sasa hakuna mchezaji aliyeweza kufikia au kuivunja  rekodi hiyo lakini hakuna pia Mchezaji aliyeweza kufikisha mabao hata 40 kwenye mashindano yote.

Msimu huu wachezaji watatu wanakuja Kwa kadi na pengine wanaweza wakavunja rekodi ya Cristiano Ronaldo ambaye aliweza kufunga mabao hayo 42 katika mechi 49

Harry Kane wa Tottenham Hotspur ana mabao 35 mpaka sasa kwenye mashindano yote

Mohammed Salah wa Liverpool yeye mpaka sasa mabao 32 kwenye mashindano yote.

Sergio Aguero wa Manchester City ameendelea kuwa na msimu mzuri akiwa ameshapachika mabao 30 msimu huu.

SWALI LINABAKI JE WATAWEZA KUIFIKIA REKODI YA RONALDO?
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini