Idadi ya Watanzania Ambao Huambukizwa Virus vya Ukimwi Kwa Siku


Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania 225 huambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU) kila siku, hiyo ikimaanisha kwamba kwa mwezi watu 6,750 huambukizwa VVU na kwa mwaka ni watu 82,125.

Takwimu hizi zimebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko leo Jumanne Machi 6, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa programu bora za Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI.

Dk. Maboko amesema kuwa, asilimia 40 ya maambukizo mapya hutokea kwa vijana wenye umri Kati ya miaka 15 hadi 24 na kati yao wengi ni wanawake.

Hii inamaanisha kwamba katika hiyo asilimia 40 ya vijana waliopata maambukizi mapya, asilimia 80 ni wanawake, amesema Dk. Maboko.

Comments
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini