Kuna wakati itakulazimu kutoa huduma/kufanya kazi bila MALIPO yoyote au kwa Malipo Kidogo Sana,sio kwa sababu unachofanya hakina thamani bali ni kwa sababu watu hawajaiona thamani bado.
Siku zote kumbuka uwezo/kipaji ulichonacho kina hatua kubwa tatu:
1.KUGUNDUA:
Kipaji/eneo lako:Hapa kazi kubwa ni kujitambua na kama haujajitambua hakuna atakayekutambua.
2.KUNOA UWEZO WAKO:
Hapa kazi kubwa uliyonayo ni kuongeza thamani na mara nyingi utakuwa unafanya mambo nyuma ya PAZIA.Mara nyingi watu watakuwa hawakuamini sana na it atakuja Ufanye mazoezi ya Muda mrefu kuongeza thamani YAKO.Kipindi hiki unatakiwa utafiti nafasi sio kwa sababu unataka KULIPWA bali kwa sababu unataka KUJINOA.
3.KUUZA UWEZO/KIPAJI CHAKO
Hapa ndio sasa unaanza kubadilisha huduma/ujuzi/Kipaji chako na Fedha ambazo watu wako tayari Kukulipa.
Unatakiwa uanze na wale ambao wameshakukubali na kukuamini.Hata kama una maono makubwa sana, uwe tayari kuanzia chini huku unaongeza thamani YAKO
UKO HATUA GANI?
See YouAt The Top
@JoelNanauka
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments