Kituo kikubwa cha runinga duniani chatoa pongezi kwa Diamond Platnumz


Kituo cha runinga cha kimataifa cha ‘BET ‘ kimetoa pongezi kwa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz baada ya album yake mpya ya ‘A Boy From Tandale’ kuingiza nyimbo tano zinazosikilizwa zaidi kwenye mtandao was iTunes nchini Burkina Faso.


Diamond Platnumz

Kituo hicho kimetoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika |”Hongera Diamond Platnumz kwa kuingiza nyimbo tano zinazosikilizwa zaidi nchini Burkina Faso kwenye mtandao wa iTunes”.


BET International ðŸŒŽ @BET_Intl
Congratulations @diamondplatnumz for having the first 5 songs on the Burkina Faso iTunes Top Songs list


Jumatano Machi 14, 2018 Diamond Platnumz alizindua album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ jijini Nairobi nchini Kenya.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini