Mama Maggie apewa tuzo ya heshima kwa kuanzisha taasisi ya kikristo kwenye nchi ya kiislamu.

Na mwandishi wetu,

Mwanamke mmoja mwenye asili ya kimarekani, ambaye ameyatoa maisha yake kusaidia makumi ya maelfu ya watoto masikini nchini Misri amepewa tuzo maalumu ya heshima na chuo kikuu kinachojulikana kama Biola University kilichopo kusini mwa mji wa Califonia. 

Maggie Gobran, anayejulikana zaidi kama “Mama Maggie,” ni mwanzilishi wa taasisi ya watoto iitwayo Stephen’s Children, ikiwa ni taasisi pekee mjini Cairo inayofanya kazi ya kuwahudumia watoto waliotelekezwa. 

Chuo Kikuu cha Biola kimetoa pongezi na tuzo hiyo wakati wakisherehekea tuzo maalumu zinazofahamika kama Charles W. Colson Courage and Conviction Award katika mahafali ya 89 yanayofahamika kama Annual Mission Conference yaliyofanyika jumatano ya wiki hii.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

share

The post Mama Maggie apewa tuzo ya heshima kwa kuanzisha taasisi ya kikristo kwenye nchi ya kiislamu. appeared first on Gospo Media.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini