Maskini Mtoto Afariki Baada ya Kuibwa Akiwa Ndani ya Gari

Maskini Mtoto Afariki Baada ya Kuibwa Akiwa Ndani ya GariKutoka nchini Uingereza polisi wanachunguza kisa cha mtoto wa miaka miwili kufariki baada ya kukutwa akiwa ndani ya gari ambalo limekutwa limedumbukizwa mtoni.

Inaelezwa kuwa mtoto huyo Kiara Moore alifariki akiwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Wales katika jimbo la Cardiff baada ya kuokolewa kutoka kwenye gari hilo.

Polisi wameeleza kuwa mama mzazi wa mtoto huyo aliripoti kuwa watu wasiojulikana waliliiba gari lake katika eneo la Emlyn hilo huku likiwa na mtoto huyo ndani na ndipo likakutwa limedumbukizwa kwenye mto Teifi siku ya jana March 19, 2018.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini