MBARAZA WA MKOA WA PWANI RAMADHAN MLAO AWAHAKIKISHIA VIJANA NA WA MAFIA KULIFANYIA KAZI MGOGORO WA HIFADHI ZA BAHARI NA WANANCHI KWA KUWAZUIWA KUVUA SAMAKI.

 Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao,akizungumza na wajumbe wa baraza la UVCCM wa Wilaya ya Mafia kuhusu kupeleka sehemu husika mgogoro wa wananchi na hifadhi ya bahari pamoja na kuwahimiza wanakipigania chama kishinde uchaguzi ujaowa serikali za mitaa. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Makwiro na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki.Picha Zote na Elisa Shunda
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

NA ELISA SHUNDA,MAFIA.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa Mkoa wa Pwani,Ramdhan Mlao amewahakikishia vijana wa Wilaya ya Mafia (Kisiwa) kulifanyia kazi suala la mgogoro uliopo katika ya hifadhi ya bahari na wananchi wanaoishi katika wilaya hiyo ambayo inajumuisha na visiwa vidogo vya Chole,Jibondo na Juani (Visiwa vidogo) kwa kulifikisha jambo hilo kwa viongozi wanaouhusika.

Akijibu Swali lililoulizwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Chole,Khamisi Musa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana CCM wilaya hiyo aliyeuliza kuhusu mgogoro wa wananchi hao kuzuiliwa kufanya shughuli za uvuvi wa samaki kwa kuwa maeneo hayo kwa sasa yamechaguliwa kuwa hifadhi za bahari kulingana na samaki aina ya Papa waliopo katika maeneo hayo ambapo Mbaraza Ramadhan Mlao alisema kuwa ameyapokea malalamiko yao na kuwaahidi kulifikisha jambo hilo katika sehemu husika ili kusaidia vijana,wananchi hata chama chake cha CCM.

“kwa historia tuliyoipata pamoja na nyie kutueleza hapa hili tatizo lina muda kidogo lakini pia  kuna athari kubwa kwa watu wa mafia na pia litatuathiri sisi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama hatutalifanyia ufumbuzi yakinifu ili watu hawa waweze kuishi salama katika maeneo yao upo mgogoro mkubwa baina ya hifadhi ya bahari na wananchi  mgogoro huu kimsingi kama isipopazika sauti kwa viongozi kwa mustakabali mema kwa mujibi wa watu wa mafia basi kisiwa hiki hakitakuwa salama wenzetu hawa wa hifadhi ya bahari wanaonekana tatizo lakini suluhu si kulikimbia tatizo suluhu ni kukaa pamoja wao na nyie mnahitajiana watu wa hifadhi wanawahitaji na nyie mnawahitaji pia kwa kuwa nyie ndiyo wenye mafia yenu lakini katika bahari hii ushuru unapatikana hivyo tatizo hili ni lazima lisuluhishwe mapema” Alisema Mlao.

Mbaraza Mlao amesema atayapeleka changamoto hizo kwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani ni msikivu na mchapakazi akaongeza kuwa atampelekea msisitizo kuona picha ya ukubwa wa tatizo hili kwa kuwa kati ya wahusika wa jambo hili yeye na wizara hii ni wahusika muhimu katika kulitatua mgogoro huu.

Aidha Mbaraza Mlao aliongeza kwa kusema kuwa watahakikisha jambo hilo linapata ufumbuzi kwa kuwa kama mgogoro huo usipofanyiwa kazi vijana hao watapata shida kukinadi Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi suluhisho ni kulifanyia ufumbuzi suala hilo kwa kuwa kama wasipolitatua jambo hilo itafika wakati wananchi watawauliza kama mmeshindwa kututatulia mgogoro huu wa hifadhi za bahari tutawaamini vipi wakati jambo hili mmeshindwa kututetea.

“Lengo la dhamira yetu ni kusaidiana na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na usalama katika maeneo yao hatuwakatai ndugu zetu wa hifadhi za bahari  lakini tunataka kwenye maisha haya kila mmoja aishi kwenye eneo lake akiwa salama salmini na afurahie maisha ya uishi wa Utanzania wake tumelipokea jambo hili tunalifanyia kazi ndugu viongozi mtapata majibu juu ya jambo hili” Alisema Mlao.

Pia Mbaraza Mlao amewakumbusha viongozi wa umoja wa vijana kuanzia ngazi ya wilaya,kata,mitaa na shina kuwajibika kwa nafasi zao walizonazo kwa kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kwa kufanya vikao na kufanya tathimini ya uhai wa chama pamoja na kuingiza wanachama wapya ambao ndio uhai wa chama.

Shirika la Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) walifika kufanya majaribio ya kuhifadhi mazingira ya kingo za bahari na samaki Papa aina ya Potwe wanaopatikana kwenye Kisiwa cha Mafia kupitia visiwa vyake vidogo ambavyo ni Chole,Jibondo na Juani mwaka 1995 kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi na kuwaahidi kuwapatia vifaa vya uvuvi,Mkataba wa miaka 10 ulipoisha wa WWF Serikali kupitia wizara husika wakatunga kanuni ya kuendesha hifadhi hiyo ambayo ndo inaleta mgogoro kwa wananchi.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini