Mimi Mars Afunguka Kuhusu Ujauzito wa Vanessa Mdee

Mimi Mars Afunguka Kuhusu Ujauzito wa Vanessa Mdee
Msanii Mimi Mars amefunguka sababu ya Vanessa Mdee kuzushiwa kuwa ni mjamzito.

Muimbaji huyo ambaye ni ndugu na Vanessa Mdee ameiambia Funiko Base ya Radio Five kuwa ulaji wa Vanessa ni miongoni mwa vitu vilivyopelea watu kuhisi hivyo.

“Hapana haiwezi kutokea, namuona kila siku ni kwamba anakula sana, mahaba ni mengi kwa hiyo wanafurahia lakini hakuna kabisa (mimba),” amesema Mimi Mars.

Vanessa Mdee yupo katika mahusiano na muimbaji mwenzie, Jux.

Licha ya kufanya vizuri katika muziki na kutokea familia moja, Vanessa na Mimi Mars hawajawahi kutoa wimbo wa pamoja zaidi ya kushirikishwa na ndugu yao mwingine anayefanya muziki wa Injili, Nancy Hebron katika wimbo uitwao Beautiful Jesus.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini