NI ZAMU YA MAN UNITED, ROMA KLABU BINGWA ULAYA LEO

Manchester United itakuwa katika uwanja wa Old Trafford kuwakabili Sevilla katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Sevilla utakaofanyika usiku wa leo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Hispania wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana hivyo kila mmoja ana nafasi ya kusonga mbele hatua inayofuata.

United itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mabao 2-1 dhidi ya Liverpool wikiendi iliyopita katika mchezo wa ligi hali ambayo itaongeza hamasa hii leo.

Vijana hao wa Jose Mourinho wamekuwa wakitumia vizuri uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford kitu ambacho Sevilla inayonolewa na Vincenzo Montella inapaswa kuwa makini.

AS Roma itakuwa nyumbani kucheza na Shakhtah Donetsk wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 walichopata kwenye mchezo wa kwanza nchini Ukraine.

Wenyeji Roma wanahitaji kupata ushindi wa bao moja ili kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Tayari timu hiyo za Real Madrid, Manchester City, Juventus na Liverpool zimetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini