SIKU NNE TU ZA KOMBE LA DUNIA KUMPA MOURINHO BILIONI 5 RUSSIA


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kulipwa Paundi milioni 1.71 Sawa na bilioni 5.3 za Kitanzania  Kwa siku nne tu atakazokuwa mchambuzi kwenye fainali za kombe la dunia nchini Russia kupitia kituo cha luninga cha nchi hiyo RT.


Mourinho alikua akiwindwa na vituo vingine kama BBC na ITV lakini akaamua kuingia makubaliano na kituo hicho kinachojulikana kama Russia's International news Channel RT ambacho hakina Haki ya kurusha matangazo moja Kwa moja.


Mkataba Kati ya kituo hicho na Mourinho ni yeye kuwepo Russia Kwa siku nne za michuano hiyo mikubwa katika ngazi ya nchi upande wa Soka ili afanye uchambuzi wake.


Mwaka 2014 Mourinho alifanikiwa kupata Paundi milioni 1 wakati alipofanya uchambuzi katika mtandao wa Yahoo.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini