SIMBA YAIKOMALIA SIMBA AL-MASRY, MVUA YAWAOKOA WAARABU.

Vinara wa ligi kuu Soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba jana usiku wametoka sare ya bao 2-2 na Al-Masry ya Misri katika mchezo wa raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho barani Afrika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mvua kubwa iliyoambatana na radi ilisababisha mchezo huo kusimama Kwa takribani Kwa dakika 30 baada ya umeme kukatika pia uwanjani Ikiwa ni dakika ya 83 wakati huo tayari matokeo yakiwa ni sare ya bao 2-2 na baadae mchezo uliendelea kumalizia dakika zilizobaki.

MCHEZO WENYEWE
Simba walianza mchezo huo Kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 9 tu ya mchezo likifungwa na Nahodha John Bocco Kwa penati baada ya Mohammed Koffi wa Al-Masry Kuunawa mpira na mwamuzi kuamuru kupigwa penati hiyo.

Dakika mbili baadae Al-Masry walifanikiwa kupata bao la kusawazisha kwa shuti Kali likifungwa na Ahmed Goma shuti lililomshinda kipa Aishi Manula na kujaa nyavuni baadae mnamo dakika ya 26 Al-Masry walipata bao la pili Kwa njia ya penati kufuatia James Kotei wa Simba Kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo ilifungwa kiufundi na Ahmed Abdalraof.

Mpaka Mapumziko Simba tayari walikua nyuma Kwa bao hizo mbili lakini kipindi cha pili Kocha wa Simba alifanya mabadiliko ya kuwatoa Yusuph Mlipili na nafasi yake kuchukuliwa na Said Ndemla pia akamtoa John Bocco nafasi yake ikachukuliwa na Laudit Mavugo.

Mabadiliko hayo yaliwapa nguvu na kasi zaidi Simba kwani waliweza kusogea mbele zaidi na kushambulia huku Emmanuel Okwi akikosa nafasi kadhaa na hatimaye dakika ya 73 Simba ikafanikiwa kupata bao la Pili Kwa njia ya penati  likifungwa na Emmanuel Okwi baada ya Mohammed Koffi tena wa Al-Masry Kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Matokeo hayo yanawafanya Simba sasa kuhitaji  ushindi wowote ugenini siku 10 zijazo jijini Cairo Misri ili kuweza kutinga hatua inayofata.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini