Wakulima wa Kahawa waiangukia Serikali

Wakulima wa zao la kahawa, Mbozi mkoani Songwe, wameiangukia serikali kuitaka isimamie ipasavyo agizo la Waziri Mkuu linalotaka kahawa iuzwe kwa mnada kupitia ushirika na kusema kupinga agizo hilo sio msimamo wao bali ni wakulima wachache wanaotumika.

Hayo yamebainika katika ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Marry Mwanjelwa ambaye awali amekutana na umati wa wakulima na wadau wa kahawa mjini Vwawa, walioeleza namna agizo hilo litakavyo poromosha maendeleo ya zao hilo kutokana na wakulima wachache kutumika na na wafanyabiashara wa zao hilo.

Dkt. Marry Mwanjelwa baada ya kujiridhisha ameagiza mjadala wa agizo la Waziri Mkuu ufungwe mara moja na kuwatoa hofu wananchi kuwa agizo hilo halitabadilishwa kwa kuwa serkali ina mpango wa kulinda maslahi mapana ya mkulima na kuondoa urasimu kwenye zao la kahawa.

The post Wakulima wa Kahawa waiangukia Serikali appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini