Wito wa Nape Nnauye Kwa Wabunge Wengine Kuhusu Uchunguzi wa Kutoweka Kwa Rais


Mbunge wa Mtama, Nape Nnauy ametoa wito kwa wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao wamuunge mkono Mbunge wa Nzega Mjini, Hussen Bashe.

Nape ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi ambao hawawezi kufika bunge, hivyo ni vyema wabunge wote wakamuunga mkono Bashe kwani hoja binafsi ni moja ya njia ya kupata suluhisho la matatizo ya wananchi.

“Kazi ya mbunge ni pamoja na kuwasemea wananchi ambao kwa namna moja ama nyingine hawana fursa ya kwenda wenyewe Bungeni. Tumuunge mkono Mhe. Bashe bila kujali tofauti zetu za Itikadi, Dini au Rangi! Hoja binafsi Bungeni, ni moja ya njia za kutafuta ukweli na suluhisho!”

Mbunge Hussein Bashe aliwasilisha bungeni taarifa ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi katika mkutano ujao wa Bunge la 11 akitaka kuundwa kwa kamati ya kibunge ili kuchunguza matukio ambayo yamekuwa yakitokea nchini na kutishia usalama wa taifa, umoja wetu na utu wa Mtanzania.

Mbunge wa CCM ataka kuchunguzwa kwa matukio yanayotishia usalama
Bashe katika barua yake alisema miongoni mwa matukio ambayo kamati hiyo maalum itachunguza ni pamoja na, kusinyaa kwa demokrasia nchini na haki za raia, kupotea, kutekwa na kuuawa kwa raia, kupigwa risasi kwa raia ndani ya nchi, matumizi mabaya ya sheria.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini