CAF Yamfungia Maisha Refa Aden Marwa Kujihusisha na Soka

CAF Yamfungia Maisha Refa Aden Marwa Kujihusisha na Soka
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limempiga marufuku ya maisha mpiga kipenga kutoka Kenya Aden Marwa kutoshiriki katika mechi yoyote ya soka.

Uamuzi huo umetolewa baada ya refa huyo kunaswa kwenye video kwenye makala ya uchunguzi akipokea pesa kutoka kwa mwandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mashindano ya kombe la Dunia Urusi.

Marwa, alichaguliwa kuismamia mechi katika mashindano hayo , na alitemwa kutoka orodha ya mashindano hayo baada ya uchunguzi huo wa Anas.

Shirikisho la kandanda Barani Afrika CAF pia limechukua hatua dhidi ya marefa wengine 10, waliopigwa marufuku kwa kati ya miaka miwili na miaka 10.

Uchunguzi huo uliofanywa na mwanahabari mpekuzi Anas Aremeyaw Anas kutoka Ghana, ulimuonyesha Refa wa Kenya Aden Marwa akipokea dola 600 kabla ya kusimamia mechi nchini Ghana, kitendo kilichofanyika kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia Urusi.

Alijiondoa kutoka usimamizi wa mechi katika mashindano hayo chini Urusi, ambapo alichaguliwa kama mmoja wa wapiga kipenga wasaidizi.

Na sasa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limempiga marufuku ya maisha kushiriki shughuli zozote za kandanda.

Aidha wengine kumi na mmoja wamesimamishwa kazi kwa muda wakisuburi vikao vya nidhamu.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini