ALIYEKUWA dereva wa Rais Trump wa Marekani, aitwaye Noel Cintron, anadai marupurupu mengi yakiwemo kuongezwa mshahara, kulipwa kwa kazi za muda wa ziada, na mengine, kutokana na kumfanyia kazi kwa zaidi ya miaka 20 hadi alipoingia Ikulu mwaka 2016.
Katika mashitaka aliyofungua, Noel anasema alikuwa akilipwa Dola $62,700 kwa mwaka na mnamo 2008 alilipwa Dola 68,000, na akapata nyongeza nyingine mwaka 2010 ambapo Trump hakumwongeza tena.
Ameongeza kwamba pamoja na mshahara huo kufikia Dola 75,000 kwa ongezeko la kawaida, alilazimishwa kulipia gharama za afya za kampuni la Trump Corporation ambazo zilifikia Dola 18,000 kwa mwaka.
Anadai pia amefanya kazi za ziada kwa muda wa saa 3,300 mnamo miaka sita iliyopita, na hivyo kwa mahesabu hayo anadai kulipwa kiasi cha Dola 178,000.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments