“Kamishna sikupongezi, nakuhurumia sana”-JPM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemtaka Kamishna mpya wa Magereza kuwatumia wafungwa katika ujenzi pamoja na uzalishaji kwa manufaa ya jeshi hilo na taifa kwa ujumla.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli .

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaapisha Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Naibu katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Martine Kasike ambao aliwateua hivi karibuni.

Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuona Jeshi hilo linaomba msaada kwa serikali kwa ajili ya bajeti ya chakula na ujenzi wa nyumba za watumishi wakati wana watu ambao wanaweza kuwatumia.

“Maana ya kufungwa ni ukafanye kazi, maaskari magereza kazi yao ni kuwafanya wafungwa wafanye kazi, ndio maana wengine wanahukumiwa na kuchapwa fimbo ziwachangamshe wakafanye kazi”, amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa, “Ni suala la aibu nchi kuendelea kulisha wafungwa, maeneo ya magereza ni mengi mno ukienda kule Mbeya mashamba yanalimwa robo tu, kila mahali kuna magereza na maeneo ya mashamba, lakini kila mwaka kunakuwa na maombi ya bajeti kulisha wafungwa”.

Aidha Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kumtaka Kamishna Jenerali wa Magereza kuzuia wafungwa kuendelea kupata huduma ambazo ni kinyume cha sheria ya magereza ikiwa ni pamoja na masiwasiliano ya simu.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini