Mahakama ya wilaya ya Mbozi imeshindwa kutoa hukumu ya kesi inayomkabili Mbunge wa jimbo hilo, Ndg. Pascal Haonga (CHADEMA) baada ya kudaiwa kwamba mchakato wa hukumu haujakamilika kulingana na uzito wa kesi.
Hukumu hiyo imeahirishwa na Hakimu Mfawidhi, Nemes Chawi anayeendesha kesi hiyo ambapo amepanga kuifanyia maamuzi Kesi hiyo namba 117 ya mwaka 2017 Agosti10.
Katika kesi hiyo Haonga na Katibu wake Wifred Mwalusanya na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kalasha, Mashaka Mwampashi wanakabiliwa na mashitaka matatu ikiwa ni pamoja na kufanya vurugu wakati wa uchaguzi na kuwazuia askari polisi kutekeleza majukumu yao tukio walilolifanya Agost 28, 2017.
Naye Wakili upande wa utetezi Bonifasi Mwabukusi ameishukuru Mahakama kwa uamuzi huo na kuamini kuwa mahakama itatenda haki.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments