Mahakamani Kisutu ambapo Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ilala (RCO), Davis Msangi ameeleza kuwa hajawahi kumuhoji Rais John Magufuli jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yaliyotamkwa na mbunge wa Kawe Halima Mdee dhidi yake.
RCO Msangi ameyaeleza hayo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati alipohojiwa na Wakili wa Mdee, Peter Kibatala.
Akimuhoji shahidi huyo Wakili Kibatala alimuuliza Msangi kuwa anamfahamu John Magufuli na anaishi wapi….? alijibu kuwa anaishi Ikulu.
Pia wakili Kibatala alimuuliza shahidi huyo kuwa uliwahi kwenda kumuhoji jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mdee kwa sababu yeye ndiyo muhanga.
RCO Msangi alijibu kuwa hajawahi kwenda kumuhoji wala hakutumia taratibu zozote za kumuhoji.
Pia RCO Msangi amedai kuwa hafahamu msimamo wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na kauli ya Rais Magufuli kuhusu watoto wa kike waliopata mimba shule wasirudishwe shule.
Pia RCO Msangi alipoulizwa kwamba Mdee alikaa muda gani chini ya ulinzi, amedai kuwa sio kwa zaidi ya Saa 48, ambapo alifikishwa Polisi July 4,2018 ila tarehe kuondoka haijui.
Baada ya shahidi huyo kumaliza kuhojiwa na Wakili Kibatala, Hakimu Simba amesema kesi hiyo imeshatimiza mwaka mmoja na ilipaswa iwe ishatolewa hukumu, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi August 7 na 8, 2018 ili kuendelea na ushahidi.
Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa July1 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni ni kuwa Rais John Magufuli “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments