Mke wa Mzungu wa Nisha Afunguka Mazito Baada ya Kuibiwa Mume

Mke wa Mzungu wa Nisha Afunguka Mazito
BILA shaka una hamu ya ubuyu! Wiki hii nakuletea wa msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye wiki iliyopita aliachia picha mbalimbali kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram zikimuonyesha akiwa na Mzungu aliyejulikana kwa jina la Anatoly Shmakov, huku akijinadi kuwa ndio mpenzi wake wa sasa na baada ya siku kadhaa zikasambaa picha za Mzungu huyo akiwa na familia yake.


Gazeti hili baada ya kuona mapichapicha hayo kwenye mtandao, lilimsaka mke wa Mzungu huyo ambaye anajulikana kwa jina la Felister James, ili kumsikia anazungumziaje kuhusu picha hizo za mumewe na Nisha?

HUYU HAPA ANAFUNGUKA:

Wikienda: Ningependa kufahamu picha ambazo zinasambaa kwenye mtandao wa kijamii zikimuonyesha mumeo na Nisha wakiwa kwenye mahaba unazifahamu?

Felister: Kwanza mimi sikuona picha hizo mwanzo, ila nilipigiwa simu na rafiki yangu yupo Zanzibar na kuniuliza kama nimeziona hizo picha mtandaoni.

Wikienda: Baada ya kuziangalia ikawaje?

Felister: Kwa kweli nilishtuka sana baada ya kuziona picha hizo kama mke na yule ni mume wangu imeleta shida sana kwenye familia.

Wikienda: Kwa sasa hali ikoje?

Felister: Nilijaribu kumuuliza mume wangu kuhusiana na picha hizo na yeye ilimshangaza kwani alipokuja Nisha nyumbani kwangu, alimuomba awe kwenye video ya wimbo wake na zile picha zipo kwenye video ya huo wimbo lakini haikuwa makubaliano ya kutangaza vile mitandaoni kuwa ni mwanaume wake. Sijapenda kwa kweli alivyofanya.



Wikienda: Lakini kwa sasa hivi vipi mpo sawa na mumeo?

Felister: Sasa hivi tupo sawa tumeyamaliza kifamilia maana ilikuwa ni tatizo sana.

Baada ya kuzungumza na mke wa Mzungu huyo lilimtafuta Nisha ambapo kila alipopigiwa simu hakupokea wala kujibu meseji.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini