Baada ya Drama za mahusiano yao kwenye mitandao ya kijamii kati ya mwanamuziki Moni Centrozone na mpenzi wake Nai hatimaye wameamua kuanza upya na kurudisha mahusiano yao ambayo yalipitiwa na jini mkata kamba aliwafanya wawili hao kutoelewana.
Nai na Moni walionekana wakiwa wanakula bata weekiend hii na kuweka wazi kuwa wapo safi na yalikuwa ni mambo ya ndani na kudai kuwa kukwazana ni mambo ya kawaida katika mahusiano na sasa wameyamaliza na wanaishi vizuri.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments