Peter Msigwa Msigwa Awapa Vidonge Wanasiasa Wanaoshindwa Kufanya Siasa Kisa Katazo la Mikutano

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji. Peter Msigwa ameweka wazi kwamba kama kuna mwanasiasa atakayekuwa anashindwa kufanya siasa kwa sababu ya kuwepo na sheria za kufanya mikutano basi mtu huyo atakuwa mwanasiasa dhaifu.

Mch. Msigwa ameyasema hayo wakati akijibu swali la www.eatv.tv kuhusu viongozi wengi kukimbilia mitandaoni kufanya siasa je, ni kutokana na masharti yaliyowekwa katika ufanyaji wa mikutano ya kisiasa. (Mikutano ifanywe ndani ya jimbo na Mbunge husika).

Amesema kwa upande wake kuwa mitandaoni hajaanza katika kipindi hiki ambacho mikutano ya hadhara kumekuwa na masharti ila alishaanza kitambo na hata kwenye jimbo lake bado ameendelea kuwa maarufu kutokana na kushirikiana na wananchi wake.

"Mimi nipo mitandaoni siku nyingi sana, natumia mitandao yote ya kijamii, hivyo sijajiunga kipindi hiki cha zuio sijajua kwa upande wa wenzangu. Na kwa upande wangu hata kama wamezuia mikutano kwenye jimbo langu bado nipo 'popular', nafanya mikutano ndani ya jimbo kwa raha zangu, na kitaifa mimi ni miongoni mwa Wabunge wachache wanaosikika kwa sababu siogopi kitu," Mch. Msigwa.

Ameongeza
 "Ni mwanasiasa ambaye atakuwa dhaifu sana akisema kwamba ameshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wananchi ili asikike kutokana na kwamba mikutano ya kisiasa imezuiliwa. Palipo na mzoga ndipo panakuwa na Tai wengi hivyo kama una hoja, hoja yako itasikika tu pamoja na changamoto za kisiasa tulizo nazo".


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini