Rais wa Uturuki Amteua Mkewe Kuwa Waziri wa Fedha

Rais wa Uturuki Amteua Mkewe Kuwa Waziri wa Fedha
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameteua baraza la mawaziri linalomjumuisha mkwe wake.

Katika baraza hilo jipya, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Sheria, Abdulhamit Gul na Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu wamebaki katika nyadhifa zao.

Akitangaza baraza hilo, Rais Erdogan ambaye aliapishwa jana kuwa rais wa kwanza mwenye madaraka makubwa nchini humo alisema mkwe wake,  Berat Albayrak ameteuliwa kuwa waziri wa fedha.

Chini ya mfumo mpya wa rais mwenye madaraka makubwa, mawaziri hawawezi kuwa wabunge, kumaanisha kuwa mawaziri hao wote wanne wataachia viti vyao.

Pia, amemteua mkuu wa jeshi Hulusi Akar kuwa waziri wake mpya wa ulinzi. Akar alikuwa mkuu wa jeshi wakati wa jaribio la mapinduzi la Julai 2016 lililofanywa na kundi la wanajeshi.

Kuna wanawake wawili pekee katika baraza lake alilopunguza kutoka mawaziri 21 na manaibu watano wa waziri mkuu. Fuat Oktay ameteuliwa kuwa makamu pekee wa rais.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini