Sababu za Mtatiro kuwa kiongozi CUF


NA FATUMA MUNA
Baada ya Jumuiya za Vijana za CUF (JuviCUF) wilaya za Dar es Salaam, kumshambulia Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa chama hicho, Julius Mtatiro na kwamba cheo alichonacho hakijulikani ndani ya CUF, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande amepangua tuhuma hizo -


na kusema kwamba cheo hicho ni halali ma  Mtatiro siyo mtu wa kwanza kuwa na cheo hicho.

Akipangua tuhuma hizo  wakati akizungumza na www.eatv.tv, Mbarala Maharagande amesema kwamba cheo alichonacho Mtatiro kipo kisheria na kinakubalika ndani ya chama kwa kufuata muongozo wa Baraza Kuu la Ungozi Taifa na kwamba kiliundwa baada ya Prof. Lipumba kujiuzulu nafasi yake.

Amesema Baraza Kuu CUF la uongozi wa taifa limetoa mamlaka ya kuundwa kamati pale ambapo itaonekana kwamba inahitajika na lilitoa muongozo  wa kuundwa Kamati hiyo  ya Uongozi baada ya Lipumba kujivua Uongozi wa CUF mwaka 2015.

Ameongeza kwamba wanaompinga Mtatiro sasa walikuwepo wakati Kamati ya uongozi inaundwa na walikubali lakini hata hiyo kuundwa kwa Kamati hiyo ni sehemu ya kutekeleza katiba ya chama na sera zake.

Akizungumzia kuhusu Mtatiro kuchaguliwa kuongoza Kamati hiyo , Maharagande amesema  "Awali, aliyekuwa Mbunge wetu wa Afrika Mashariki, Twaha Taslima ndiye alikuwa Mwenyekiti kwenye Kamati hiyo lakini baadaye ikaonekana kwamba anastahili kugombea Uenyekiti wa chama lakini ilishindikana baada ya mKutano wetu wa Uchaguzi kuvamiwa na Prof. Lipumba na watu wake pale Ubungo".

Ameongeza, kwamba Kamati hiyo ingeweza kuundwa hata kama Mwenyekiti angekuwepo, iwapo tuu Baraza lingetoa muongozo hivyo Mtatiro anapaswa ajulikane kama kiongozi kwani ni mwaka wake wa pili anaongoza kamati iyo.

Mwenyekiti wa JuviCUF wilaya ya Ilala, Canal Kitimai kwa niaba ya viongozi wenzake wa wilaya mapema wiki hii alisema kwamba Mtatiro siyo mwanachama wa chama hicho na kwamba alikwishavuliwa uanachama na kuongeza kwamba anashangaa cheo alichojipa kwani chama chao hakikitambui.

EATV
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini