NDEGE iliyotengenezwa na kampuni ya Boeing 787 ya Marekani ambayo ni moja ya ndege zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania, ni ndege ya kimapinduzi ambayo ina kila aina ya starehe katika safari zake kwa madaraja yote.
Ni ndege ambayo haina kelele zozote ukiwa ndani, hii ni kutokana na injini zake zisizokuwa na makelele makubwa kutokana na mfumo wa kuzuia sauti kuwafikia abiria.
Baadhi tu ya zana za starehe katika ndege hiyo iliyotengenezwa Marekani na kuwekewa injini aina ya Rolls Royce za Uingereza ni viti vya kuvutia ambavyo ‘vinakunjulika’ na kulazwa kama kitanda, nafasi kubwa ya kunyoosha miguu na televisheni kubwa za inchi 23 zilizo mbele ya abiria.
Miongoni mwa sababu kubwa za abiria kuipenda Dreamliner Boeing 787 ni:
• Nafasi kubwa zilizomo ndani yake. Hii ni pamoja na madirisha makubwa na dari iliyo juu zaidi, hii huwapa fursa abiria wake kujiona wako mahali pa wazi zaidi na hivyo kutokuwa na woga wowote. Hii ni pamoja na nafasi ya juu ya kuweka mizigo midogo ya mikononi.
A flight attendant checks out the seating options of
• Usingizi mzuri wakati wa safari. Kwa vile 787 huruka juu katika kiwango cha futi 6,000 kutoka ardhini badala ya futi 8,000, uvutaji wa pumzi unakuwa rahisi ambapo mapafu ya abiria yanapokea oksijeni zaidi na hivyo kulala vizuri zaidi, kuzuia maumivu ya kichwa na kuvuta pumzi vizuri.
Kwa vile ndege imetengenezwa kwa mchanganyiko wa madini na vyuma mbalimbali badala ya ‘aluminum’, Boeing huongeza unyevu zaidi katika hewa kuliko ndege zingine. Hivyo, njia ya hewa kupitia puani haiwezi kukauka kirahisi au kukuletea harara, hivyo hali hiyo hukufanya ulale vizuri zaidi.
• Usariri usiokuwa na mitingishiko. Boeing 787 imeundwa kwa kila aina ya utaalam wa kisasa wa kuzuia mitingishiko wakati wa usafiri. Hii ni tofauti na ndege za aina nyingine ambazo huwa na mitingishiko hususan zinapopita juu ya maeneo fulani.
• Madirisha yenye mwanga maalum wakati wa kulala. Boeing 787 ina madirisha maalum yanayoendeshwa kielektroniki ambapo yanaweza kufanywa yakawa ya giza ili kuruhusu abiria kulala kama vile ni waati wa usiku, hivyo kukwepa kusumbuliwa na mwanga.
• Maliwato murua. Maliwato ndani ya Dreamliner yana kila sifa nzuri; mabomba na zana za kusafishia uchafu kirahisi, sehemu ya kukalia inayojifunga na kufunguka kwa kutumia nyenzo zilizopo.
• Mfumo mzuri wa matangazo. 787 ina mfumo wa vipaza sauti ambavyo ni rahisi kusikika na kueleweka.
• Ndege yenye nakshi na burudani za kutosha. 787, hususan 787-9, ambayo ina urefu wa futi 20 zaidi kuliko 787 ya mwanzo, inavutia kwa nakshi na mapambo mbalimbali ndani yake kiasi cha kuwaliwaza kikamilifu abiria.
Hii ndiyo Boeing 787 ambayo unaweza pia kutoa maagizo yoyote unavyotaka iwe ndani yake kwa kadiri ya utashi wako mnunuzi.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments