Msanii wa bongo fleva DIAMOND PLATNUMZ ambaye kwa sasa yupo nchini marekani amewataka wazazi wenzake ambaye ni Hamissa Mobetto na Zari kuondo matabaka kati yao ili waweze kuwakuza vyema watoto wake na kuwafanya waishi kwa ushirikiano pale watakapokuwa.
"Nawapenda watoto wangu wote mama zao watabaki kuwa rafiki zangu na washkaji zangu sipendi nikionekane nikiwa na Hamissa au Zari iwe Big ishu sitaki iwe ivyo kwasababu wote ni wazazi wenzangu ninachokitaka kuona wazazi wenzangu kuacha tofauti na kushirikiana ili siku kukitokea kitu kama birthiday ya mtoto wangu basi watoto wote na familia zao wote wawepo napenda nione watoto wangu washirikiane kama ndugu bila matabaka" Diamond
"Nawashukuru wazazi wenzangu kwa malezi mazuri ya watoto wangu ila wanachotakiwa si kuwatengenezea upendo kwangu mimi ila na bibi yao na ndugu zao lakini hata miongoni mwao sababu maisha yenyewe mafupi" alisema Daimond
Daimond amesema kuwa anafanya kazi ili kuwaaandalia maisha mazuri ili mwisho wa siku wawe viongozi na wasimamizi wa vitu anavyovipambania leo wakiwa wanaungana kwa pamoja.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments