Tanzania yaongoza kwa Hili Afrika Mashariki


Mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwaka unaoishia mwezi Juni mwaka huu umeendelea kushuka kutoka asilimia 3.6 ilivyokuwa mwezi Mei hadi asilimia 3.4, huku sababu kuu iliyochangia kushuka huko ikiwa ni kupungua kwa kasi ya bidhaa zisizo za vyakula.


Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo amesema hali ni tofauti kidogo kwa nchi za Kenya na Uganda ambako mfumuko wa bei umepanda kiasi.

“Kupungua kwa mfumuko huo kumechangiwa na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula ambazo ni Bia kwa asilimia 1.1, gharama za ukarabati wa vifaa vya umeme na viyoyozi kwa asilimia 1.8, gesi za kupikia majumbani kwa asilimia 5.6, majiko ya mkaa kwa asilimia 2.0 na gharama za mawasiliano kwa asilimia 2.6”, amesema Kwesigabo.

Aidha, Kwesigabo amesema fahrisi za bei nazo zimeongezeka huku akizitaja bidhaa zilizochangia kushuka huko kuwa ni gharama za ukarabati wa vifaa vya umeme na viyoyozi, gesi ya kupikia, majiko ya mkaa pamoja na gharama za mawasiliano.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini