Waandaaji Miss Tanzania wajibu tuhuma zilizotolewa na Miss Arusha


Mkurugenzi na mtayarishaji wa shindano la Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi amekanusha tuhuma zilizotolewa na mshindi wa taji la Miss Arusha kuwa sio za kweli kwamba hawamkufahamisha zawadi watakazo mpatia zaidi ya stakabadhi ya fedha taslimu kama alivyodai wakati akihojiwa. 

Basilla amebainisha hayo wakati akizungumza na eatv.tv baada ya kuwepo malalamiko kutoka kwa washiriki wa shindano hilo akiwemo mshindi wa taji la Miss Arusha kuwa hajui chochote kuhusu zawadi anayopaswa kupatiwa tofauti na stakabadhi ya fedha aliyopatiwa. 

"Sisi tumewaandaa mawakala ambao watatangaza zawadi kabla ya wiki ya mashindano, hivyo wakati huo wa mwisho ndipo washindani wa taji wanaambiwa zawadi ni nini. Huwezi kushiriki mashindano bila kujua nini utapata, kama amesema zawadi pekee aliyokuwa akiijua ni stakabadhi ya fedha taslim basi hiyo ndiyo zawadi yake na pengine iliyomo asiyoijua ni zawadi ya ziada kwa ajili yake”, Basilla mwanukuzi. 

Hata hivyo, shindano la kumtafuta Miss Tanzania bado linaendelea katika ngazi ya mikoani ambapo imepita na kupata washindi wa mataji katika mikoa ya Dodoma, Rukwa ,Mwanza, Tabora, Ilala na hivi sasa linaelekea Morogoro. 

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini