Watoto mapacha walioungana Maryness na Anisia Beatusi, wamepelekwa nchini Saudia Arabia kwa matibabu baada ya kupata ufadhili kutokana na uhusianao mzuri baina ya serikali ya Tanzania na nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Saudia Arabia nchini Mohammed El Malik amesema mfalme wa saudia amewafadhili watoto hao baada ya ombi lilitolewa na serikali ya Tanzania.
Akizungumzia upasuaji huo daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Petronila Ingiloi amesema kuwa wamepata ugumu hasa kwenye matokeo ya mwisho baada ya kufanikisha upasuaji wa watoto hao.
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji watoto, Zaituni Buhari ambaye anaye safiri na watoto hao amesema uchunguzi wa awali utafanywa kwa umakini ili kuweza kufanikisha upasuaji salama kwa watoto hao.
Msilikize hapa chini daktari Zaituni akielezea zaidi juu ya upasuaji wa hao watoto mapacha walioungana.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments