Waziri Mwakyembe atoa nafasi kwa wasanii na Basata kujadili tozo ya milioni 5 (Video)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezungumza na wadau wa sanaa wakiwemo wasanii wa muziki kujadili sakata jipya la tozo ambalo limeanzishwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Moja kati ya tozo ambazo zimechukua muda mwingi kujadiliwa ni tozo ya milioni 5 kwa kila kampuni ya biashara ambazo zitataka kufanya kazi na wasanii.

Baada ya kikao hicho Waziri Mwakyembe aliwataka wasanii wachache pamoja na wadau wa sanaa wakae na Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kujadili namna kubadili huo mfumo.

 VIDEO:

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini