Msanii wa muziki Bongo, Hamonize amefunguka kuhusu wimbo wa Diamond Platnumz 'Jibebe' alioshirikiana na Mbosso na Lava Lava kukutana na ule wake, Atarudi.
Muimbaji huyo kutokea WCB amesesema nyimbo hizo zinafanya vizuri kutokana na ukweli kwamba mashabiki wameamua kuwa nao na si kwamba wanajua sana.
"Kabisa siumeona mwenye balaa la Jibebe lakini nashukuru watu wanatusapoti sana sio kwa sababu sisi tunajua sana, watu wamemua tu kutusapoti WCB fo life," Harmonize ameiambia Wasafi TV.
Katika hatua nyingine Harmonize amefunguka kuhusu kuanzisha Band yake na sababu ya kufanya hivyo pia.
"Konde Music Band itakuwa na bei zake, ukisikia Harmonzie anatumbuiza kwa Band lazima hela itakuwa ni tofauti, so tutegemee vitu vizuri tu nachukua muda mwingi kufanya mazoezi kuzipitia nyimbo zangu vizuri, ikifikia siku nikatumbuiza mtu asiboreke apate ladha zaidi," amesema Harmonize.
Harmonize ni miongoni mwa wasanii walioshiriki kwenye Listening Party ya Albamu ya Barnaba inayokwenda kwa jina la Gold.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments