Huyu Mbwana Samatta Hashikiki Tena Ubelgiji..Atupia Tena

Nyota ya mshambauliaji wa Tanzania na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta inazidi kung’aa akiichezea timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji katika michuano ya UEFA Europa League ya kuwania kuingia hatua ya makundi.

Samatta baada ya kufunga hat-trick mchezo uliyopita, usiku wa August 30 alishuka tena uwanjani wakiwa ugenini nchini Denmark kurudiana na Brondby IF, kutokana na mchezo wa kwanza kushinda kwa magoli 5-2, game ya leo walikuwa wanahitaji sare au ushindi wowote au wafungwe kwa idadi ndogo ya magoli.

Wakiwa ugenini KRC Genk wamefanikiwa kuingia hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2018/2019 kwa kuifunga tena Brondby IF kwa magoli 4-2, magoli ya Genk yakifungwa na Malinovsky dakika ya 14, Ndongala dakika ya 32, Dewaest dakika ya 66 na Mbwana Samatta dakika ya 87.



Hivyo Genk wanafuzu hatua ya makundi kwa jumla ya aggregate magoli 9-4, Mbwana Samatta akiweka rekodi ya kuifungia Genk katika game 6 mfululizo akiwa leo kafunga goli lake la tisa katika game sita, hiyo ni habari njema na sasa Genk wanasubiri droo ya makundi kujua watapangiwa group gani
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini